0
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amewafunda wajumbe wanawake wa Bunge Maalumu la Katiba dhidi ya vitendo vinavyoweza kuwavunjia heshima na kuwaambia Ukimwi upo na umekithiri. Makinda, ambaye hiki ni kipindi chake cha nane akiwa bungeni, alitoa hadhari hiyo jana mjini hapa kwenye semina ya wajumbe wanawake wa Bunge hilo.
Akisisitiza juu ya nafasi ya wajumbe hao kuhakikisha kipengele cha usawa wa kijinsia wa asilimia hamsini kwa hamsini kinaingizwa kwenye katiba, alisema sauti zao na hoja zao zitasikika na kuchukuliwa kwa umakini kutokana na kujiheshimu.
Alisema amekaa kipindi hicho kirefu bungeni pamoja na baadhi ya wabunge wanawake, kutokana na kujiheshimu. Alitaja mwingine ambaye wamekaa pamoja muda mrefu ni Anna Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake.

Spika Anne Makinda.

Katika semina hiyo iliyoandaliwa na Tanzania Women Cross Party Platform (T-WCP Uliongo), Makinda alisema, “Niliingia mdogo kama wadogo wengine hapa, lakini nilijiheshimu… Ukijiheshimu unachokisema watakuamini,” alisema Makinda.
makinda
Anne Makina

Atahadharisha kuhusu Ukimwi.

Alihadharisha wajumbe hao wa Bunge Maalumu dhidi ya Ukimwi akisema, “HIV ni rampant (umekithiri) hapa…umekuja kwa kazi maalumu, haya mengine yanakupata vipi?” Alisema Ukimwi upo hivyo wawe makini isije baada ya Bunge kumalizika, wakatoka wakiwa wamepata matatizo.
“Uende bunge la katiba urudi na matatizo. Umekuja kwa kazi maalumu haya mengine yanakupata vipi?” alihoji.
Spika alisema kitendo cha wanawake kutojiheshimu na hatimaye kutoa mwanya wa kuandikwa kwenye magazeti ya udaku, hoja yao ya kutaka katiba itoe usawa wa hamsini kwa hamsini haiwezi kuungwa mkono.
Kwa mujibu wa Makinda, yuko mbunge mmoja (bunge la kawaida) alikuwa akichangia hoja ambayo ilikuwa nzuri lakini alipozungumza, aliambiwa hayo maneno akamwambie fulani; wakimaanisha aliye kwenye uhusiano naye.
“Tukiwa na nidhamu sisi, hoja zetu zitakubalika,” alisema. Naye Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake Tanzania, Anna Abdallah alisisitiza akisema, “tunaomba tutunze heshima ndiyo ustawi wa mwanamke. Hapa kuna vivutio vingi.”

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X