Baadhi ya vitu alivyokuwa navyo Sharon:
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Sharon Justice Laiza, mkazi wa Kilimahewa jijini Mwanza amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha baada ya kudondoka ghafla akiwa njiani kueleakea kwa mgonga wake aishiye Kiseke, Ilemela Mwanza...
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea juzi saa kumi
na moja jioni , mwanamke huyo alidondoka umbali wa mita kadhaa
kabla ya kufika kwa mganga wake.
Baada
ya kudondoka, mwanamke huyo alilazimika kumpigia simu mganga
huyo maarufu kwa jina ustaadhi akimtaarifu kuwa amedondoka
kabla ya kufika na kwamba anahitaji msaada....
Taarifa
zinaarifu kuwa, Mganga huyo alituma vijana wake wakamchukue kwa
kuwa yeye hakuwa nyumbani wakati huo. Vijana walifika na
kumbeba, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo mwanamke huyo,
vijana wale walilazimika kumpigia simu mganga wakimtaka aje
haraka kwa kuwa hali ya Sharon haikuwa nzuri....
Akisimulia
tukio hilo, mganga huyo alidai kuwa baada ya yeye kurudi
nyumbani, hali ya mwanamke huyo ilikuwa ni mbaya zaidi kiasi
cha kushindwa hata kuleza shida iliyompeleka kwake.
"Niliporudi
hakuweza kunieleza shida yake kutokana na hali yake.
Nilimuuliza nikusaidiaje, akasema nipeleke Hospitali ya Mwananchi.
"Tulimpeleka
lakini wakasema wao hawana sehemu ya kumlaza wakasema twende
Bugando. Pale Bugando walisema alikuwa amebanwa na kifua na
miguu ilikuwa imekufa ganzi , hivyo akalazwa.
"Wakati
huo alikuwa anaongea kwa shida. Aliniagiza niende kazini kwake (
New Mwanza Hotel ) nikatoe taarifa na kisha nirudi kesho yake
asubuhi maana wakati huo ilikuwa ni usiku wa saa nane.
"Kabla
sijaondoka, Daktari alinambia kuwa mgonjwa anataka maji.Nikaenda
katika duka la Bugando kuangalia lakini wakati narudi nikakuta
ameshafariki dunia....
"Baada
ya tukio hilo, nilirudi na kutoa taarifa kwa balozi na kesho
yake asubuhi tukatoa taarifa kwa serikali ya mtaa na polisi." Alisema mganga huyo
Akiongelea
kuhusu uhusiano wake na mwanamke huyo, mganga huyo alidai kuwa
amejuana naye alipomfuata akiomba msaada wa kupata kazi.
"Tulifahamiana
naye baada ya kuomba nimsaidie apate kazi baada ya kufukuzwa
alipokuwa hapo mwanzo. Nilifanya mipango yangu, akapata kazi New
Mwanza Hotel. Sikuwahi kumtibu ugonjwa wowote mbali na msaada
wa kupata kazi"
Wakiongea
na mtandao huu, afisa mtendaji wa Kiseke, bi Hellen Mcharo na
mwenyekiti wa mtaa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Bugando ukiwasubiri
ndugu zake toka Arusha.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment