
Yohana anasema katika maisha yake
amekuwa ni mwenye hofu kubwa baada ya kukumbwa na tukio hilo la aina
yake la kukatika miguu akiwa usingizini. Anasema hadi sasa haelewi namna
hasa tukio hilo lilivyomtokea, kwani hakuhisi maumivu yoyote .
Anasema tukio hilo la aina yake
lilimtokea mwaka 1992, lakini halikuwahi kuandikwa wala kutangazwa,
badala yake ni watu wachache waliokuwa wakilifahamu.
Anasema siku hiyo usiku alikwenda kulala kama ilivyo kawaida, alipoamka asubuhi alikuta miguu yake imekatika.
Kilichomshangaza zaidi ni kwamba
hapakuwa na damu wala jeraha lilionekana. Palionekana pana kovu, kana
kwamba alikatika mguu muda mrefu uliopita.
Anasema mara ya kwanza ulianza
kupotea mguu wa kulia, hiyo ilikuwa ni mwezi Machi, 1992. Kutokana na
tukio hilo, ndugu zangu walifanya jitihada mbalimbali ikiwemo kufanya
maombi katika nyumba mbalimbali za ibada, huku wengine wakienda kwa
kuwaona waganga wa jadi.
“Kama binadamu wa kawaida ilichukua muda sana kuamini kilichotokea ndani ya maisha yangu na mguu wangu,” anasema.
Mwezi mmoja baadaye yaani mwezi
Aprili mguu wa kushoto nao ulikatika katika mazingira yaliyo sawa na
yale ya awali.Inaweza kuwa vigumu kuamini lakini ulimwengu ndivyo
ulivyo.
Anakumbuka mazingira ya kukatika
kwake yanahusishwa na imani za kishirikina kwa sababu siku chache
zilizopita kabla ya kukumbana na dhahama hiyo aliwahi kukorofisha na mtu
katika vilabu vya pombe za kienyeji anayesadikiwa kufanya tendo hilo.
Baada ya miaka saba kupita Yohana
alipelekwa Hospitali Teule ya Ikonda wilayani Makete kupata huduma za
tatizo lake. Alifanikiwa kupata msaada wa baiskeli ya magurudumu, ambayo
aliitumia kwa miaka mitano.
Kwa sasa baiskeli hiyo haifanyi kazi
kutokana na watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi kuiba matairi na vyombo
muhimu vinavyoiwezesha baiskeli hiyo kufanya kazi.
Pamoja na kupewa baiskeli hiyo na
wasamaria wema, Yohana anakiri pia kuchongewa viatu na hospitali hiyo
ambavyo vinamuwezesha angalau kutembea umbali mfupi.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment