0
chadema

CHADEMA

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinaynga kimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wawili katika manispaa ya Shinyanga kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na madai kuwa  viongozi ngazi ya taifa  wa chama hicho kundekeza  majungu,migogoro ,kudhalilisha baadhi ya viongozi  pamoja na  kuwapa majina ya wasaliti wa chama.
Madiwani  waliofikia maamuzi hayo magumu ni diwani wa Kata ya Ngokolo Sebastian Peter maarufu OBAMA WA NGOKOLO na Zacharia Mfuko wa kata ya Masekelo  ambao wamesema wameamua kufikia maamuzi hayo magumu kama ishara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho kitaifa.
chadema

Madiwani wa CHADEMA

 
Madiwani hao wawili tayari wameshakabidhi barua za kung’atuka nafasi zao katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
 
Hili   ndiyo barua ya tamko la diwani wa Ngokolo Sebastian Peter kuhusu kujiuzulu nafasi yake ya udiwani aliyoikabidhi ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga ikielez sababu za kuchukua maamuzi hayo huku akisisitiza kuwa atabaki kuwa mwanachama mwadilifu wa Chadema
CIDM1
CIDM2

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X