0


ayy 
Ukimzungumzia Ay unazungumzia moja kati ya wasanii kutoka Tanzania wanaopeperusha vizuri bendera ya Tanzania,kwa kufanya Collabo na wasanii mbalimbali wa kimataifa ambaye pia kwa Lebo yake ya Unit Entertainment inamsimamia Stereo na Ommy Dimpoz.
Millardayo.com imepata nafasi ya kuongea na Ay kuhusu mipango yake ya mwaka mpya wa 2014 alianza kwa kusema>> ‘Binafsi nataka kutoa kazi kwa ajili ya wapendanao,ujumbe uliopo ndani ya hii ngoma ni ujumbe ulio imara uko ‘strong’ ni ujumbe unaoweza kumwambia mtu yoyote kuna mistari mingine utaisikia utaona ni ya wapendanao kama wapenzi na kuna mingine utaisikia ya vitu vingine’
‘Naamini hiyo ngoma ni classic na itaishi miaka yote maana mapenzi hayaishi kwanza na tunaishi kwenye hayo mapenzi,nategemea kutoa januari mwishoni au February mwanzon kabla ya valentine ngoma hii inaitwa Ahsante’.
Ay amesema ngoma hiyo amefanya kwa Marco Chali kutoka Mj Records.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X