KESI iliyokuwa ikimkabili Padri Deogratius Makuri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida kushindwa kutoa fedha za matunzo kwa mwanawe, jana ilifikia ukingoni baada ya mlalamikiwa kuamua kulipa jumla ya Sh 580,000 taslimu ikiwa ni gharama za matunzo, matibabu na mavazi kwa ajili ya mtoto huyo.
Kiasi
hicho cha fedha kilikabidhiwa kwa mlalamikaji Maria Boniphace na dadake
Padre ajulikanaye kwa jina la Bahati Michael mbele ya Hakimu wa
Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini Singida, Ferdinand Njau.
Awali
Hakimu Njau aliionesha barua kutoka kwa Padri Makuri ambapo alisema
hawezi kufika mahakamani hapo kutokana na kile alichodai ni sababu
zilizokuwa nje ya uwezo wake.
Katika
barua hiyo, Padri Makuri amekiri kuwa jukumu la kumtunza mtoto huyo ni
lake na kwamba kutokana na sababu hiyo muhimu ameamua kutuma mtu alete
fedha ya matunzo kwa mtoto wake.
Kati
ya fedha aliyoleta mahakamani hapo, alisema kuwa Sh 480,000 ni matunzo
kwa miezi sita kuanzia Des 10, 2013 hadi Juni 10, 2014 ikiwa ni Sh
80,000 kila mwezi ambapo Sh 100,000 ni kwa ajili ya matibabu na gharama
ya mavazi kwa mtoto huyo.
Hakimu
Njau amemtaka mlalamikiwa kuleta kiasi hicho hicho tena hapo ifikapo
Juni 10, mwaka huu vinginevyo kesi itafufuliwa. “Ilichokuwa inataka
Mahakama hii ni fedha za matunzo kwa mtoto huyu, basi .... hilo sasa
limefanyika.
"Sioni
sababu ya kuendelea na shauri hili labda hapo mlalamikiwa
atakaposhindwa kuheshimu amri ya Mahakama.” alisema Hakimu Njau
aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo.
Padri
Makuri, ambaye alikuwa Katibu wa Askofu Jimbo Katoliki Singida kabla ya
kuingia kwenye kashfa hii, anatuhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minane (jina limehifadhiwa) aliyezaa
na Maria Boniphace (26), mkazi wa eneo la Mitunduruni mjini Singida
ambaye anadai alikuwa mfanyakazi jimboni hapo.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment