
Mbunge wa Nyeri Mjini Esther Murugi. Picha/JOSEPH KANYI
Na EVALYNE GITHINJI
Bi Murugi
alisema kisa hicho kilitokea siku mbili kabla ya kisa ambapo mwanamke
alipoteza mwanawe aliyedunda sakafuni alipokuwa akijifungua.
“Nilimtembelea
wifi yangu katika hospitali hiyo alipokuwa ameenda kujifungua. Hakuweza
kujipindua kitandani baada ya kujifungua. Hata shuka zilikuwa
hazijaoshwa. Ilinibidi mimi na familia yangu kuziosha shuka hizo,”
akasema.
“Sio muuguzi
aliyetuhudumia bali ni mwanafunzi wa uuguzi. Baada ya kumuuliza kwa nini
jamaa wetu hakuwa ameshughulikiwa, alisema mama akizaa mtoto ni wake,”
akaongeza mbunge huyo ambaye zamani alikuwa waziri.
Hata hivyo
mkuu wa hospitali hiyo Bw Cyrus Njoroge alimfahamisha Bi Murugi kuwa
angejaribu kuyapeleka malilio hayo katika ofisi zao kuu ili kuhakikisha
jambo kama hilo limetatuliwa.
Alieleza kuwa baada ya wifi yake kutoka hospitalini, siku tatu hazikuisha kabla ya kisa hicho cha mama kupoteza mtoto kutokea.
Bi Charity
Wanjiku mwenye umri wa miaka 27, alimpoteza mwanawe alipokuwa
akijifungua mnamo siku ya Januari 15 katika hospitali hiyo ya Nyeri.
Bi Wanjiku
alilalamika kuwa mtoto huyo alifariki kufuatia kutoshughulikiwa vyema na
wauguzi alipokuwa anajifungua kwani badala ya kushauriwa vyema
walimuachilia kujifungua kama amesimama.
Familia ya Bi Wanjiku inangojea ripoti kamili kuhusu tukio hilo kutoka kwa wizara ya afya iliyofanya uchunguzi.
Bi Murugi pia
alionya jinsi serikali haina wafanyikazi wa afya wa kutosha haswa
kufuatia tangazo la wauguzi kugoma baada ya siku 14, kama hospitali za
umma hazitawaajiri wauguzi zaidi.
Alisema kuwa ni jambo la huzuni jinsi wagonjwa wanatatizika kufuatia ukosefu wa wauguzi wa kutosha.
Kulipwa vyema
“Hakuna yule
anaweza kuwalaumu wafanyikazi wa afya ambao hutafuta kazi nje ya nchi
kwani huko wanalipwa vizuri, serikali yetu inafaa kuwalipa vizuri,”
alisema zaidi.
Bi Murugi alisema hayo alipokuwa ameenda kumtembelea mama aliyejifungua katika hospitali hiyo na kupata pacha watatu mfululizo.
“Mimi
nilielezwa na kasisi ambaye aliona habari ya mama huyu aliyejifungua
watoto watatu lakini hana uwezo wa kifedha na nikaamua kuja kumsaidia,”
alisema Bi Murugi.
Mbunge huyo
alisema kuwa anafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba mama huyo
amesaidika kifedha kwa kutafuta wahisani wema ili kumsaidia kuwalea
watoto hao.
Bi Naomi Maina, 26, bado amelazwa katika hospitali hiyo, akingojea watoto hao kukomaa kikamilifu ndipo atoke.
Bi Maina
alijaliwa watoto hao mnamo siku ya Januari 22 na huku akiwa amejawa na
furaha alishukuru kupata msaada kutoka kwa Bi Murugi.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment