
Hoja kubwa ya msingi leo ni jinsi
gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi wake. Ikumbukwe kwamba,
hapa tunazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika uhusiano, lakini
wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya ndoa.
Leo nazungumzia juu ya wewe
ambaye upo katika uhusiano ambao haueleweki, lakini ndoa unaitaka.
Unajua cha kufanya? Soma hapa chini mambo ya kufanya ili mpenzi
uliyenaye akuoe haraka...
1.EPUKA MAKUNDI MABAYA
Mwanaume anapenda kuwa na mke
mwenye staha, ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na makundi ya
‘mashangingi’ ni alama ya kwanza kabisa kuwa unapenda au tayari una
tabia za kishangingi. Wanaume wengi hawapendi kabisa wanawake wenye
tabia za hovyo, wenye kampani ambazo si nzuri.
Lakini yawezekana, jamaa
alishakuambia juu ya kilio chake hiki, lakini wewe umekuwa kama umeweka
pamba masikioni mwako, hili ni tatizo. Linda heshima yako, kaa mbali na
makundi hatari, ili umfanye jamaa akuone wewe ni mwanamke thabiti ambaye
huigi, hushabikii na wala huna tabia mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa
mbali na makundi ya wanawake hatari!
2. ZINGATIA MAVAZI YAKO
Kila mtu anamjua mtu wake alivyo,
mwanamke hata wewe unamjua mpenzi wako alivyo. Sina shaka unafahamu
anapenda nini na nini anachukia. Unajua kabisa, nina uhakika na hilo.
Lakini pamoja na kwamba jamaa anaweza kuwa na vitu ambavyo vinamvutia
zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike, una mapendekezo yako au vitu
ambavyo unapenda zaidi kuvifanya!
Huzuiwi, lakini swali la msingi,
mwenzi wako anapenda? Kama wewe unapenda sana skin jeans na top
inayoacha kitovu nje, yeye hapendi kwa sababu ana nia ya kukufanya mke
hapo baadaye. Sasa utakuwa mke gani ambaye hata Salim anaona sehemu zako
za faragha hadharani?
Ukiachana na chaguo la mwenzi
wako, lakini lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa mtu, ujitambue!
Jisitiri vyema. Kwani kuna urembo gani wa kuvaa nguo inayoonesha mwili
wako ulivyo? Kuna burudani gani kuacha nyeti zako wazi? Unataka nani
akuone ulivyo? Mke hana sifa hiyo dada yangu, sasa ili uweze kuwa na
sifa hii muhimu, lazima uzingatie sana mavazi yako.
3. JIPE MOYO
Hili nilishawahi kulizungumza
sana katika mada zilizopita, baadhi ya wanawake wamekuwa wakikatishwa
tamaa na rafiki zao au watu wengine wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya
kuolewa au watahangaika sana lakini hawatapata mume, kisa eti HAVUTII!
Mwingine anajinyima mwenyewe
nafasi akisema; “Mimi nina balaa, sina bahati ya kuolewa, ndiyo maana
wadogo zangu wote wameolewa nimebaki mimi.”
Huu ni uvivu wa kuwaza. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa unaitengeneza wewe mwenyewe.
Unaitengeneza kwa misingi ya
kwanza, kujipa moyo mwenyewe kwamba wewe ni mzuri na una sifa na haki za
kuolewa kama wanawake wengine. Jipe moyo mwenyewe, huna nuksi wala
balaa, wewe ni mzuri na una sifa za kuwa mke hapo baadaye.
Iko hivi, ukianza kujishusha
mwenyewe, ni dhahiri kwamba hata mavazi yako hayatakuwa mazuri, uso wako
hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na matumani moyoni, hapo sasa ni
mwanzo wa kuzorota afya yako. Utapata mchumba kweli? Utasubiri sana kwa
mtindo huo.
4. ACHA PAPARA
4. ACHA PAPARA
Haizuiwi kuuliza kuhusu
mustakabali wa uchumba wenu, lakini ni vizuri basi kuwa na kiasi.
Kuuliza kila wakati au kuwa mtu wa kulaumu, hakutakusaidia kumfanya
jamaa achukue maamuzi ya haraka ya kukuoa na badala yake yanaweza kumpa
picha tofauti.
Ni rahisi kuwaza kwamba, unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo hutakuwa na staha tena. Kuwa mjanja, achana na papara. Usilogwe ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako, halafu ndiyo umuulize; “Sasa honey, mbona hata huzungumzii ndoa yetu? Hivi utanioa kweli? Eeeh baby? Niambie basi mpenzi wangu
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment