Mcheza filamu Zuberi Mohamed‘Niva’ juzi alijikuta akipata fedhea baada
ya kupigana na mtu inayesemekana kama ni mpenzi wake, sakata hilo la
aibu lilitokea katika Hotel ya Ndeka iliyopo maeneo ya Magomeni, tukio
hilo lilitokea mida ya saa tano usiku.Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa
Niva alikuwa kapanga katika Hoteli hiyo na baadae alikuja na binti huyo
na kuagiza chakula na kupelekewa chumbani huko ambako ugomvi ulitokea
na kusababisha vurugu zilimfanya Niva kutoka nduki.
Kufuatia
ugomvi huo uliotokea ghorofa ya tano chumba namba 5, msanii huyo alitoka
nduki akiwa na nguo ya ndani tu na kukimbia hadi chini na kutoweka
jambo lilofanya wahudumu kuingia katika chumba hicho na kushuhudia
uharibifu uliofanywa na wapenzi hao, huku kuta za chumba hicho zikiwa
zimetapakaa kwa uchafu wa vyakula.
Msanii hiyo katika tukio hilo
amepoteza vito vya thamani kama vile saa, mkufu, simu na vitu
vinginevyo, hadi habari hizi zisizo na shaka zinatufikia msanii huyo
alikuwa hapatikani katika simu yake ya mkononi, ili aweke wazi
kilichopilekea ghafla na mpenzi wake kugeuzaa Hoteli ulingo wa masumbwi.
KWA HISANI YA FC
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment