![]() |
| Vincent Kigosi ‘Ray’. |
“Kuna baadhi yetu wamekuwa wakikaa vikao ili kutaka kumweka pembeni Ray kwa kuwa ameshindwa kuleta umoja ndani ya Bongo Movie na amekuwa akifanya mambo yasiyokubalika…” alisema mmoja wa wasanii ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Chanzo hicho kimesema kwamba wasanii wasiomtaka Ray wamekuwa wakiweka vikao usiku katika kumbi mbalimbali za burudani za jijini Dar kwa ajili ya kumng’oa kwenye cheo hicho.
Wasanii wanaomkubali Ray wanadai anastahili kuendelea kuliongoza kundi hilo kwa kuwa ana msimamo thabiti na hakuna mwingine anayeweza kuliongoza.
Msanii wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere, amesema uongozi wa Ray unafika kikomo na wanatakiwa kumchagua kiongozi mpya au kuendelea naye na jukumu hilo liko mikononi mwa wasanii wenyewe.
“Kimtazamo Bongo Movie linaenda vibaya na hii siyo kwa sababu ya Ray, bali wasanii wote ni jukumu letu kulijengea heshima kundi hilo, katika uchaguzi wa leo Ray anaweza kuchaguliwa au asichaguliwe kwani kura ni demokrasia…” alisema Steve Nyerere.
Ray hakuweza kupatikana mara moja kuuzungumzia mpasuko huo ndani ya Kundi la Bongo Muvi.
GPL

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment