MTU mmoja m kulima na mkazi wa eneo la Kumsenga wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, aliyefahamika kwa jina la Yusuph Pascal, ameuawa kwa kupigwa na vitu mbalimbali katika tukio linalodaiwa kuwa ni fumanizi la mapenzi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa Kigoma, Fraisser Kashai alisema mjini hapa kwamba
mtuhumiwa huyo wa fumanizi, aliuawa mwanzoni mwa wiki hii.
Alisema
baada ya kifo chake, mume wa mwanamke aliyefumaniwa kwa kushirikiana na
watu wengine, waliuchukua mwili wa marehemu na kuutupa eneo la Mnarani
mjini Kasulu.
Kufuatia
tukio hilo, kamanda huyo alisema watu watano wanashikiliwa na jeshi
hilo, wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo la mauaji ya mkulima huyo.
Kashai
aliwataja watu waliokamatwa kwenye tukio hilo kuwa ni watu watatu wa
familia moja, ambao ni Augustino Adrian, Laurent Adrian na Peter Adrian,
ambao ni wamiliki wa nyumba yalipotokea mauaji.
Aliwataja
wengine waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kuwa Mihosho Hamza, ambaye
ni mume wa mwanamke aliyefumaniwa akiwa ni mpangaji katika nyumba
yalikotokea mauaji na Raymond Shirima.
Akisimulia
kuhusu tukio, Mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoa Kigoma, David
Kisusi alisema awali marehemu akiwa katika nyumba ambayo mwanamke
aliyefumaniwa naye alikuwa akiishi, alivamiwa na watuhumiwa, ambao
walimpiga na vitu vizito na kufariki.
Alisema
baada ya kuona kuwa mtuhumiwa huyo wa fumanizi ameuawa, mume wa
mwanamke huyo na watuhumiwa wengine wanne, waliuchukua mwili wa marehemu
na kwenda kuutupa eneo la Mnarani ili kupoteza ushahidi.
Alisema
polisi walipofika eneo ambalo mwili huo wa marehemu ulikuwa umetupwa,
walianza uchunguzi wao na kubaini kuwa ulitupwa hapo baada ya kuuawa
eneo lingine.
Ndipo
walipofuatilia michirizi ya damu hadi katika nyumba hiyo na kukuta
katika moja ya vyumba hivyo, kuna eneo limemwagiwa mchanga mwingi ili
kuficha damu hiyo ya marehemu.
>>Habari Leo.
>>Habari Leo.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment