Huku bunge la Afrika kusini likifanya kikao maalum
cha kumheshimu Mandela, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwe ameiambia BBC
kuhusu siku za mwisho za maisha ya babaake.
Amesema kuwa ijapokuwa hakuwa akifungua macho
mara kwa mara,alikuwa na uhakika kuwa aliweza kusikia vile familia yake
ilivyompenda.
Makaziwe amekiri kuwa hakuweza kuwasiliana vyema
sana na babake na kwamba babaake hakuweza kuonyesha hisia zake,lakini
yote hayo alitaka familia yake kupatana.
Amesema kitu kikubwa alichoelimishwa na babaake ni kuwa na ujasiri wa kusamehe.
BBC
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment