Zifuatazo ni kauli za Ismail Aden Rage ambazo nimemnukuu akiongea na Waandishi kutokana na
stori zilizochukua headlines kwa siku kadhaa kuhusu Kamati kumsimamisha kama Mwenyekiti wa Simba.
1.
‘Kwanza napenda kuipongeza kamati ya utendaji ya TFF kwa kuafiki mimi
Ismail Aden Rage ndio Mwenyekiti halali wa Club hii ya Simba na nimepata
barua yao jana ileile, katika katiba ya Simba kuna kitu wengi hawajui
maana ya Kamati ya utendaji wanadhani ni wale watu saba… hapana!!!
kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti… hamna kaimu
hapo, kuna Wajumbe 7 waliochaguliwa katika mkutano halali… , Wajumbe
saba wa kuchaguliwa mmoja wapo akiwa ni Mwanamke na wengine wawili wa
kuteuliwa na Mwenyekiti, leo nitateua mwingine mmoja.. nimetoa mmoja’
2.
‘Kwa bahati mbaya Club ya Simba haina Makamu Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti alishajiuzulu ila ina Kaimu Mwenyekiti tu ila huku kwenye
katiba hatajwi, kwenye katiba ya Simba Makamu Mwenyekiti ana kazi mbili,
moja kwa kuelekezwa na Mwenyekiti na pili Makamu Mwenyekiti anafanya
kazi wakati Mwenyekiti hayupo’ – Aden Rage
3.
‘Joseph Itangire ni Kaimu Mwenyekiti tu niliemteua lakini hajapata
uhalali wa kikatiba kwa hiyo katiba hii inaendelea kusema, mwenye
mamlaka ya kuitisha kamati ya Utendaji mara nne kwa mwaka ni Mwenyekiti,
nimekua muungwana tumefanya mara 12 mwaka huu.. kama Mwenyekiti hayupo,
katiba inasema anakaimu hana mamlaka ya kuitisha kikao chochote kwa
mujibu wa katiba kwa hiyo kikao kile kilichofanyika hakina tofauti na
kikao cha harusi’
4.
‘Maamuzi yangu kama Mwenyekiti wa Simba sasa, kwa kuwa mkutano ule
ulikua ni batili… jana niliandika barua kwa TFF kwamba viongozi hawa
wamevunja katiba za TFF, Simba, CAF na FIFA… ukitaka kulalamika ni
lazima uwe na ushahidi wa aina mbili unaokubalika ambao ni document na
video casette iliyo na sura za watu na maneno yao waliyosema, wana
document ambayo kwenye barua ya Malinzi amekiri anayo na imesainiwa na
Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itangire’
5.
‘Nimesikitika sana na maagizo ya TFF ya kunitaka niitishe mkutano na
Wanachama wa Simba ndani ya siku 14, sijui wameitoa wapi kwenye katiba
ya TFF na Simba, wamekwenda mbali na kuninyang’anya madaraka… wamenipa
alafu wameninyang’anya alafu wamenipa na Ajenda ya mkutano, sasa
wamenirudishia madaraka ya nini? mimi kama Mwenyekiti wa Simba… siitishi
mkutano, nalindwa na katiba kwa hilo’
6.
‘Unaponipa amri unaninyang’anya madaraka yangu, katiba inasema kama
naona itafaa nitaitisha… tuheshimu katiba, nilitegemea taarifa ya kwanza
ya TFF mpya ingelaani mapinduzi ya kipuuzi yanayotokea’
7.
Heshima yangu mimi ni Mbunge taifa linaelewa hivyo, nimekuta ofisi hii
hakuna umeme miaka 18 pamoja na pazia za magunia, nimekuta uhuni mtupu..
wachezaji wameuzwa, Henry Joseph, Matole na wengine uliza wanachama wa
Simba ilipata shilingi ngapi? leo imani inawatoka kusikia nimeuza
Wachezaji wawili tu Congo DRC milioni 320 na nikaweka wazi hadharani sio
kuwaambia Mke wangu na watoto wangu..
8.
Leo nimetumiwa msg kutishia kuuwawa na tayari nimesharipoti Polisi, leo
hii msg nimepata mtu kaniambia ‘Nisipotoka Simba ataniua’ alivyokua
mpumbavu hajui hizi simu zinasajiliwa, nimecheki jina lake mpaka mtaa
anaokaa pengine sasa yuko Lupango… why??? mpira ni burudani!! kuna mtu
alikua Simba sasa yuko TFF anataka kuleta vurumai ndani ya TFF na Simba,
kwa nini? kwa nini ununue watu? waandishi wa habari hebu tuache
kuchochea, wewe Mwandishi ni nani ununuliwe? kuna Mwanamke Mwaandishi
mmoja kalipwa milioni 2 ili anichafue, sijali.. ‘
9
Nimefanya Demokrasia sana na ndio inanitokea puani, nimeteua kamati…
ziko kamati nyingi sana lakini sijaona Mwandishi hata mmoja anakwenda
kuuliza kamati ya ufundi, Usajili ila kila mmoja ananishambulia mimi,
leo sitaki maswali ya Waandishi wa habari, sasa mna hiari… kuandika au
kuacha wala hamnipi tabu nyie, kuchafuliwa nimezoea’
10. Ukitaka kuwa kiongozi teka Ikulu kwanza, hapa
Home
»
ENTERTAINMENT
»
SOKA
» KAULI 10 ZA ADEN RAGE BAADA YA KUTIMULIWA SIMBA ZIKO HAPA.SINA MBAVU KWA KWELI.HATARI TUPU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment