Omar Faraji Nyembo 'Ommy Dimpoz'.
KUONYESHA jinsi gani alivyojipanga
kuporomosha burudani ya kufa mtu
katika Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, msanii mahiri
wa Bongo Fleva, Omar Faraji Nyembo 'Ommy Dimpoz' amewaambia mashabiki
wake wote wakutane Dar Live siku ya Jumatano.
Mkali
huyo aliyekuwa nchini Marekani atapiga shoo Dar Live Jumatano ambayo ni
Sikukuu ya Eid sambamba na Mwamba wa Kaskazini, Joh Makini. Kupitia
akaunti yake ya Instagram, Dimpoz amewataka mashabiki wake kutokosa shoo
hiyo maana itakuwa ya aina yake. Ameeleza kuwa yeye pamoja na timu yake
ya Poz kwa Poz watakuwa ndani ya nyumba kuwapa raha mashabiki. Katika
sikukuu hiyo, Bendi ya Twanga Pepeta nayo itatoa burudani sambamba na
Profesa Calabash atakayewapa burudani watoto.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment