Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 17, utawala wa Rais Barack Obama umeidhinisha baadhi ya shughuli za kiserikali zisimamishwe kuanzia mapema leo baada ya Bunge la nchi hiyo kuikataa bajeti yake, wakipinga mabadiliko ya kisheria ya sekta ya afya yaliyofanyika hivi karibuni.
Huku matumaini ya suluhisho la mtafaruku
huo wa
bajeti unaopambanisha wabunge wa chama tawala cha Democrat dhidi ya
Republicans yakizidi kufifia, wachumi na wataalamu wa uongozi wameonya
kuwa uamuzi wa kusitisha huduma ‘zisizo muhimu’ utaathiri uchumi wa
Marekani kwa kiwango kikubwa.
Wafanyakazi katika vitengo mbalimbali
vya serikali
nchini humo waliodamkia maofisini leo alfajiri wamejikuta wakirudishwa
majumbani, huku karibu 800,000 kati yao wakiambiwa wachukue likizo bila
malipo mpaka muafaka utakapopatikana.
Wafanyakazi pekee watakaobakizwa ni wale
ambao
shughuli zao haziwezi simama, kama vile madaktari na manesi, waongoza
ndege na wafanyakazi wa shirika la posta la Marekani.
Katika baadhi ya vitengo kama NASA –
inayofanya
tathmini za usafiri wa kwenda sayari nyingine na anga za mbali – zaidi
ya asilimia 95 ya wafanyakazi wote wamewekwa benchi katika kipindi hiki
cha mtafaruku wa bajeti.
Vilevile huduma za utoaji hati za
kusafiri na viza
zinatarajiwa kusimama kwa kiwango kikubwa, na wasafiri toka nchi
nyingine wanaambiwa watarajie foleni ndefu kidogo katika vituo vya
uhamiaji kwa sababu wafanyakazi wengi wa kitengo hicho wamepumzishwa. (AFP)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment