
Akizungumza hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment