Ili kukabiliana na wanafunzi wapenda kuangalizia 'wapiga chapo'
katika mitihani, wahadhiri na wanachuo katika Chuo Kikuu cha Kasetsart
jijini Bangkok nchini Thailand wameamua kutumia njia hii ya kuvaa kofia
ya karatasi ili kuzuia vitendo vya kupiga chabo.
Wanafunzi hao hutumia karatasi aina ya A4 ambazo huzivaa kichwani
kama kofia na kuwafanya waone katika karatasi zao za mitihani tu bila
kupepesa macho sehemu nyingine. Alipohojiwa mmoja wa wahadhiri wa chuo
hicho aitwaye Nattadon Rungruangkitkrai kuhusu tukio hili alisema
"yalikuwa makubaliano yetu na hakuna mwanafunzi yeyote aliyelazimishwa
kuvaa kofia hiyo. Kila mmoja alikuwa na furaha wakati wa kupitishwa
utaratibu huu na wengi wao waliojiona kuwa huru zaidi katika mtihani."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment