Miaka ya karibuni tumeshuhudia jinsi biashara ya mabenki ilivyopata upinzani mkubwa baada ya mitandao ya simu kuanza kutoa huduma za kibenki kupitia simu za mikononi kiasi ambacho mtu anauwezo wa kutembea bila cash lakini pesa ikiwa kwenye akaunti yake ya simu.
Teknolojia inazidi kurahisisha huduma hiyo, sasa Kampuni ya Uniqul ya Finland imezindua kile ilichokiita mfumo wa kwanza kuwahi kutokea wa malipo kwa utambuzi wa SURA ya mteja ‘the first ever payment platform based on facial recognition’ kama ilivyoripotiwa na Dail Mail.
Kwa teknolojia hii mteja haitaji kutembea na wallet mfukoni wala kadi ya benki wala simu kwaajili ya kulipia bidhaa dukani, kinachohitajika wakati wa kufanya shopping ni kamera inawekwa sehemu ya kufanyia malipo (checkout) ambayo itakuwa inachukua picha ya mteja anayekuwa anataka kulipia bidhaa zake.
Baada ya picha kuchukuliwa mashine hiyo inafanya kazi ya kuscan katika database yake ili kuoanisha sura na taarifa za akaunti ya mteja kisha kukata kiasi anachopaswa kulipa na kupewa risiti na kuondoka, shughuli hiyo ya malipo kwa mfumo huo inaweza kufanyika kwa sekunde tano tu.
Kuhusu swala la usalama wa mfumo huo wabunifu wa teknolojia hiyo wa Uniqul wamedai kuwa teknolojia hiyo ni salama sababau inalindwa na ‘military grade algorithms’ na kuwa inauwezo wa kutambua hata tofauti ndogo za mapacha.
Msemaji wa kampuni hiyo alisema “In the background our algorithms are processing your biometrical data to find your account in our database as you are approaching the cashier. The whole transaction will be done in less than 5 seconds – the time it usually takes you to pull out your wallet”.
Teknolojia hii sio kwamba ni mawazo kwani tayari mfumo huo umeanza kutumika katika hatua za majaribio huko Finland ambapo usajili wa watu umeshaanza katika jiji la Helsinki, ili kuweza kuitumia huduma hiyo ni lazima mtu asajiliwe na kuingia katika system.
Jinsi ya kutumia mfumo huo wateja wanatakiwa kusajili ‘credit cards’ zao ili kuziunganisha na akaunti ya Uniqul.
Home
»
ENTERTAINMENT
»
KIMATAIFA
» Teknolojia mpya ya kulipia manunuzi kwa utambuzi wa SURA unaofanywa na software itakayochukua nafasi ya kadi za benki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment