0
Mwanadada wa filamu nchini, Aunt Ezekiel anatarajia kuachia wimbo wake wa kwanza unaitwao ‘Mguu kwa Mguu aliomshirikisha Linex Sunday. Wimbo huo umetayarishwa na Mr.T Touch wa Seductive Records.
page
Linex amesema kuwa Aunt Ezekiel amemchagua kufanya naYe wimbo kwasababu ni mwalimu mzuri wa muziki anayeweza kumuongoza mtu katika kipindi cha maandalizi ya nyimbo mpaka inatoka.
“Mimi ni mwalimu mzuri, niamuapo kufundisha, sipaniki kwasababu hii ni kazi yangu ambayo inaniendeshea maisha yangu, kwahiyo Aunt ameamua kunichagua mimi nifanye naye nyimbo kwasababu ameona mimi ninaweza kufanya kile ambacho anakihitaji kiwe kwenye nyimbo yake,” alisema Linex.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X