BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu.
Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha
Kalole, Tarafa ya Kisiju, walayani humo.
Kwa mujibu wa baba wa binti huyo, Omari
Salum, mwaka 2010 ndugu wa
mkewe aitwaye Nyasenene aliyekuwa akiishi Charambe Mbagala, jijini Dar
alifika nyumbani kwake na kuwaomba wampe mtoto wao kwa ajili ya kwenda
kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’.
Baada ya binti huyo kufanya kazi kwa
muda mfupi aliugua malaria, baba
mtu akapewa taarifa na kufika Dar kwa ajili ya kumuona mwanaye
aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
Mzee huyo amesema alikwenda Muhimbili na
kufanikiwa kuzungumza machache
na mwanaye huyo ambapo alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo.
Mzee huyo alisema ilibidi aondoke licha
ya mwanaye kumtaka alale
lakini kwa vile yeye ni mwanaume isingewezekana kulala hospitalini hapo.
“Kesho yake nilipewa taarifa kuwa
mwanangu amefariki dunia usiku.
Tulianza taratibu za mazishi na kumzika kwenye Makaburi ya Kichangani,
Mbagala, Dar kutokana na kukosa fedha za kuusafirisha mwili hadi
Mkuranga,” alisema mzazi huyo
Mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa
jina la Said Ali Ngaora ‘Dr. Lamba’ anayeishi Mbagala Rangi Tatu, Dar
alifika katika kijiji hicho cha Kalole mwaka huu na kuwaambia wananchi
kuwa kijijini hapo pana mtu anaonekana alikufa na kuzikwa lakini bado
yupo hai na amewekwa sehemu na kutaja gharama za kumtoa ni shilingi
milioni tatu.
Akielezea tukio zima Dr. Lamba alisema
wananchi walimruhusu akaanza kazi kwa kushirikiana na wataalamu wenzake.
Dr. Lamba na timu yake walifanikiwa
kumuibua msichana huyo
anayekadiriwa kuwa na miaka 12-15 kwenye mji ambao hakuna mtu anayeishi
akiwa ndani ya banda la kuku huku kukiwa na chungu chenye damu, asali na
udongo ambavyo vilikuwa ndivyo vyakula vyake akiwa na muonekano wa
kutisha kwa kuwa na nywele ndefu na chafu na kucha zikiwa ndefu mithili
ya jini.
Baada ya kumtoa alipelekwa katika uwanja
wa mpira kijijini
hapo na kuogeshwa pamoja na kukatwa kucha kisha akapelekwa katika nyumba
aliyofikia mganga huyo, hata hivyo hakuweza kuongea vizuri.
Kwa
mujibu wa mashuhuda ulimi wa Nuru ulikuwa mzito na mpaka sasa
anazungumza kwa vitendo kama bubu huku chakula ambacho ameanza kula
vikiwa ni ugali na kuku, uji na juisi ya embe.
Mbali na shilingi
milioni tatu za kutoa, mganga huyo anataka milioni 15 kutokana na dawa
anazompa kwa ajili ya matibabu ili arudi katika hali ya kibinadamu .
Hata hivyo, baadhi ya ndugu wanaopinga
kuwa Nuru siyo mtoto wao lakini
baba mzazi anasema ni mwanaye kutokana na alama zilizopo mgongoni mwake
na anafanana sana na mdogo wake.
Makamu Mwenyekiti wa kijiji
hicho, Ali Hassan Ndeko alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema
mpaka sasa wanakijiji wanaendelea kumiminika kwa ajili ya kumuona mtoto
huyo akiwa chini ya uangalizi maalumu wa mganga huyo huku wakijitolea
vyakula.
GPL:
GPL:




Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment