Zaidi ya watalii 1,000 na watalaam katika masuala ya matembezi ya mbugani wameshiriki kwenye survey kubwa ya aina yake kutafuta nchi bora zaidi kwa safari za mbugani. Matokeo yametoka na Tanzania imekuwa mshindi.
Ngorongoro Crater
Kwa mujibu SafariBookings.com (The largest online marketplace for African safari holidays) iliendesha utafiti wa miaka miwili kwa kuchukua maelezo kutoka kwa waendaji wa safari hizi mbugani pamoja na makampuni yanayojihusisha na kiwanda hicho kuangalia ni nchi ipi bora zaidi barani Afrika.
Ikipata nyota 4.8 kati ya nyota 5, Tanzania imeibuka mshindi kwa kuizidi Botswana kwa takriban point 10. Nchi zingine zilizoingia fainali ni pamoja na Kenya, Zambia na Afrika Kusini.
Utafiti huo ulijikita kupitia michanganuo 2,305 kutoka watembeaji wenyewe na 756 kutoka kwa wataalam kwenye industry hiyo yenye watalii wengi miongoni mwao wakiwemo waandishi wa mitandao/vitabu kuhusu masuala hayo ikiwemo Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt na Footprint.
Sababu kubwa Tanzania imechaguliwa kama nchi bora ni kwasababu ni maskani pa maeneo mawili maarufu kwa watalii duniani, mbuga ya wanyama Serengeti na Ngorongoro Crater.
Sehemu zote mbili hutoa muonekano wa kuvutia za maisha halisi ya porini kuonekana duniani.
Flamingo wa Ziwa Manyara
Pamoja na Serengeti na Ngorongoro zilizopo kaskazini mwa Tanzania, maeneo ya Magharibi na Kusini yana vivutio vingine muhimu kama hifadhi za taifa za wanyama za Gombe na Mahale huku hifadhi ya Katavi ikijulikana kwa wingi wake wa vifaru na nyati.
Home
»
ENTERTAINMENT
»
KITAIFA
» Tanzania yatajwa kuwa nchi bora kwa safari za mbugani, yazishinda Afrika Kusini, Botswana na Kenya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment