0
Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli, amezikanusha tetesi zilizoanza kuenea tangu jana kuwa amefariki kwenye ajali ya boti katika ziwa Victoria.
IMG_41701
Akiongea kwa simu na Shebby D blog asubuhi ya leo, Saida ambaye baada ya kutumbuiza kwenye tuzo za Kili wiki iliyopita alielekea Makongorosi Chunya mkoani Mbeya, amesema yupo hai na ni mzima wa afya.
“Mungu wangu, mimi niko hai, ndugu yangu, naomba uwaeleze watanzania kwamba Saida ni mzima, hakuna chochote kilichotokea hata mimi mwenyewe nimeshangaa yaani watu wanapiga simu, ni suala la msiba lakini si kweli,” amesema Saida.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X