Rapper Nay wa Mitego ni miongoni mwa wasanii waliojitokeza kulaani kitendo cha gazeti la Ijumaa lililoandika habari ya kumchafua Ommy Dimpoz kiasi cha kumfanya achukiwe na mashabiki wa muziki. Gazeti la Ijumaa liliandika kuwa Ommy alimtukana Mangwair kwa kudai kuwa alikufa maskini.
Nay Wa Mitego ameandika kupitia kurasa za Facebook na Instagram kuwa ameshindwa kuvumilia kwa kile kinachoendelea kwa mashabiki wa muziki kupoteza matumaini na upendo kwa Ommy Dimpoz ambaye wiki iliyopita alipondwa na makopo ya bia kwenye show ya Kili Tour mjini Dodoma.
“Nimesikitishwa sana na vitendo na shutuma zinazoendelea dhidi ya msanii mwenzetu OMMY DIMPOZ nimeshindwa kuvumilia inabidi niongelee hili swala Kama Ulifatilia kwa Makini alichokisema OMMY siku ya usiku wa tunzo za Kili Alisema Makampuni Makubwa yawekeze kwa Wasanii kwa sababu kazi tunayofanya ni kubwa lakini matokeo yake tunakufa Masikini…Lakini kuna watu kwa sababu zao binafsi wameamua kupandikiza Chuki kwa Kumtumia Marehemu ALbert Mangwea ili kumuharibia DIMPOZ maisha yake ya kimuziki.Watanzania tufungue Macho sio kila kinachoripotiwa kina ukweli Mnaweza kumuhukumu Mtu asiyekuwa na Hatia kisa kuna watu wametumia Mamlaka na Power zao kuangamiza wasiokiwa na Hatia Kwa maslahi yao Binafsi…..Ina maana Ndugu zangu Mnapenda wasanii wenu Tuendelee kubaki na kufa Masikini wakati kazi tunayofanya ni Nzito….Ni hayo tu,” aliandika Nay.
Home
»
ENTERTAINMENT
» Nay wa Mitego alia na gazeti lililompandikizia chuki Ommy Dimpoz kwa kudai alimtukana Ngwair
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment