0
Miaka sita iliyopita Tasnia ya filamu Tanzania ilikosa tuzo za ndani kutokana mpangilio na uendeshaji mbaya wa tasnia hiyo. Tasnia hiyo imekosa ushirikiano baina ya waigizaji, wasambazaji na wadau waliopo kwenye tasnia na kumekuwepo matabaka miongoni mwa wasanii ambapo kuna wale wenye majina makubwa, wa kawaida na wale wadogo wasio na majina.
king_of_love
Katika mihangaiko ya Shebby D Blog kutaka kujua kuna tatizo gani ndani ya tasnia hiyo iliyotoa vijana wengi katika mazingira magumu na kuwaweka katika hali mzuri ya kimaisha kupitia sanaa ya uigizaji.
Kama ilivyo katika maisha ya kawaida panapo, shindano huitajika mshindi na mtu anayeshindwa hutakiwa kukubali matokeo kwakuwa huo ndio ushindani. Hili limekuwa tatizo ndani ya tasnia ya filamu kutoka kabla ya Steps Movies Awards 2012-13 zilizondaliwa na kampuni ya Steps Entertainment kwa wasanii wanaofanya kazi na kampuni hiyo. Wasanii wa filamu walitunikiwa tuzo mbalimbali japo bado baadhi ya wasanii hawakuridhika na utoaji wa tuzo hizo. Tuzo hizo zilizofanyikia kwenye ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo jijini Dar es Saalam.
Bahati mbaya baadhi ya wasanii hawakuweza kukubali matokeo na hivyo kuzuka ugomvi kati yao na kujenga picha mbaya kwa jamii na waandaaji huku wengi wakisema kutokuwepo kwa ushirikiano na umoja miongoni mwao ndio sababu ya tasnia ya filamu kutokuwa na tuzo za kueleweka kwa wasanii wote.
Shebby D blog inawapa pongezi Steps Entertainment kwa kututoa kimasomaso cha miaka 6 bila ya kuwa na tuzo zozote zinazowekza kuonyesha tasnia ya filamu inatoka wapi na inaelekea wapi na pia kuwapa changamoto wasanii wanaochipukia kuiga mifano ya wasanii waliofanikiwa katika tasnia hiyo nchini.
Production Manager wa Ndauka Entertainment aliiambia SHEBBY D BLOG changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya filamu Tanzania, “Waandaji wa filamu na wasanii wa Tanzania tunatakiwa kuwa na ushirikiano kwanza,wenyewe kwa wenyewe na baada ya hapo ndipo twende kwenye uongozi ambao tunaupa mamlaka ya kutuongoza, kusimamia na kututetea haki zetu popote pale.”
“Tukisema tusubiri kufanyiwa kila kitu bila ushirikiano wetu hatutafika popote wataendelea kunufaika wachache ambao tayari wana majina,” aliongeza. “Sioni kama kutokuwa na tuzo za filamu Tanzania kuna madhara kwetu, tunachotakiwa kufanya ni kuboresha masoko wa kazi zetu,tukauza filamu zetu kwa pesa nzuri basi na maisha ya wasanii yatakuwa mazuri. Kwa sasa wasanii tunapata shida sana ya masoko ya kazi zao, Unakuta unatengeneza filamu kwa milioni 16, Halafu wewe unapewa milioni 20 yeye anaenda kuuza na kupata faida zaidi,au unakuta unampeleka filamu yako kwa msambazaji anakwambia kaingiza sokoni copy 10,000 kumbe ni zaidi ya hizo ambazo amekwambia.”
Dennis ameishauri serikali ijaribu kuunda sheria zitakazolinda kazi za wasanii na kulinda haki miliki za kazi za wasanii. “Serikali inatakiwa kulinda haki miliki za wasanii ili hii tabia ya wasambazaji kumiliki haki miliki za wasanii na kuwawezesha kuchukua stamp za TRA na kubandika kwenye kava ya CD ili ziwe halali kwa kuuzwa. Lakini tatizo linatokea wasambaji wanawadanganya wasanii wamechukuwa stamp 10,000 wakati wamechukua zaidi kwa manufaa yao. Kwahiyo tunaomba serikali isimamie na iunde sheria ambayo itawabana wamiliki kutomiliki haki miliki za wasanii na zimilikiwe na wasanii wenyewe.”

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X