0
Baada ya kutamba na Muziki Gani, Diamond na Nay Wa Mitego wako mbioni kuachia ngoma nyingine hivi karibuni baada ya kupembua ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’.
Cover
Nay ameiambia SHEBBY D BLOG kuwa kuna nyimbo tatu ambazo zipo tayari, Salamu Zao, Kwa Masela na Utakula Jeuri Yako, hawajajua ipi itaanza kutoka kwasababu kila mmoja yupo katika tour zinazoendelea. Wamesema wakikaa wakashauriana na wadau mbalimbali ndipo watakapoamua mzigo upi uingie mtaani kwanza.
“Kuna kazi ambazo zinakuja hivi karibuni ambazo nimefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi sijajua ni ipi ambayo itaanza kutoka lakini tutawaita wadau wachague ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’ ambazo zipo tayari na ‘Utakula Jeuri Yako’ nimefanya mwenyewe, ilibidi tutoe nyimbo ambayo tumefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi hakuna maamuzi ya moja kwa moja tuitoe au kila mtu atoe ya kwake au tutaendelea na project yetu iliyoendelea, kwahiyo wadau wakae mkao wa kula,” amesema Nay.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X