0
Muongozaji na mtayarishaji wa video zilizoshinda ama kutajwa kwenye tuzo kubwa barani Afrika na anayesifika kwa kuzipeleka video za muziki za Tanzania mbali, Adam Juma wa Visual Lab; Next Level amesema kwa sasa hafanyi tena video hizo.
Adam Juma na Addo Novemba
Amesema kwa sasa anafanya zaidi kazi na NGOs mbalimbali katika masuala ya kuelimisha jamii.
“Kusema kwamba ndio business yangu, right now am not doing, lakini kuna wasanii bado nawasiliana nao kuwasaidia kibiashara, kimaendeleo, so am still around lakini kuna vitu vingi ambavyo naviorganise, moja ni kuorganise vitu kama forums za wasanii, ndivyo vitu ambavyo naviangalia sana,” 
“Sifanyi video kibiashara, mtu akinilipa nifanye video sifanyi naye.”
Amesema haoni kama kutakuwa na pengo kubwa kwakuwa wapo vijana wengi wanaofanya video nzuri.
Unauzungumziaje uamuzi wa Adam Juma kuacha kufanya video?

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X