0
Hili ndilo tanki linalosambaza  maji mji wa Runzewe

Hizi ni baadhi ya nyumba zilizowekwa X


HII NDIO MSHINE INAYOSUKUMA MAJI

Haya ndio mazingira yaliyopo karibu na idara ya maji Runzewe

Angalia mwenyewe mfuko uliojaa mchanga ndio ushikilia bomba je ni sawa?
PICHA ZIMEPIGWA NA ALLY SHABAN 

 Wakazi wa mji wa Runzewe iliyopo Mkoa mpya wa Geita Wilaya ya Bukombe wameipenda sana huduma ya maji wanaipata.Lakini malalamiko yao wanaomba mzingira ya idara ya maji yaboleshwe zaidi kwani yamezungukwa na makazi ya watu. Pia kuna uchafu mwingi sana na kuna vyoo ambavyo kisheria havistahili kuwepo maeneo hayo.
     Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wakazi wa maeneo hayo ambao hawakutaka majina yao yaandikwe wamedai kuwa maji wanayotumia wanahisi si salama kutokana na mazingira yanapotoka.Hivyo kunaweza kutokea na mlipuko wa magonjwa kwa watumiaji, na wamesema maji hayo ndio yanatumika kwenye Hospitali yao ya kijiji, Shule ya Sekondari ya Runzewe na pia wananchi wenyewe  kwa ujumla wanatumia maji hayo. Tunaomba sana tuboleshewe mazingira kwani maji ni uhai .Ona ndugu mwandishi haya mazingira yalivyo we mwenyewe si unayaona, hayo ni maneno toka kwa mwananchi akimwambia mwandishi wetu.
       Na pia wamesema kuna baadhi ya nyumba zimewekewa X na viwanja  vya maeneo hayo watu wameambiwa wasijenge wala kuweka kitu cha kudumu na wameahidiwa watakuja kulipwa. Lakini muda umekuwa mrefu na watu wanashindwa kufanya vitu vya maendeleo .Hivyo wanatoka kujua ni lini wizara husika itafanya hivyo.
MAJI NI UHAI MAZINGIRA YANAYOPOTOKA MAJI HAYO YAWE SAFI NA SALAMA NDIO MANENO YAO WANANCHI HAO.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X