
Katika
hali isiyo ya kawaida mwanamke aitwaye Johari Raphael ( 35) mkazi wa
mtaa wa Makanyagio Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi
amejifungua mtoto wa kiume mwenye viungo vya ajabu utofauti na
banadamu wa kawaida. Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya
Mpanda
Naibu Mkongwa aliwaambia waandishi wa Habari Ofisini kwake jana kuwa
mwanamke huyo alijifungua mtoto wa ajabu ambae alikuwa na kichwa
kikubwa kama cha mtu mwenye umri mkubwa huku mikono na miguu yake
ikiwa mifupi mfano wa pingili za miwa.
Dkt
Mkongwa alieleza kuwa mwanamke huyo alijifungua mtoto mwenye uzito
wa kilo nne na nusu(4.5) hata hivyo alifariki dunia muda mfupi
baada ya mama yake kujifungua kwa njia ya upasuaji baada ya kushindwa
kujifungua kwa njia ya kawaida katika hospitali hiyo.
Madaktari
waliamua kumfanyia upasuaji baada ya kupata maelezo kutoka kwa mama
huyo alipoeleza kuwa huo ulikuwa ni uzao wake wa tano na kati ya
zao hizo amekuwamara hizo akijifungua kwa shida hali iliyo pelekea
kujifungua watoto wawili wakiwa wameisha kufa.
Dkt
Mkongwa akifafanua zaidi alieleza kuwa baada ya kupata historia ya
mama huyo waliamua kumfanyi a uchunguzi na walipobaini kuwa mama huyo
hawezi kijifungua kwa njia ya kawaida kutokana na ukubwa wa kichwa
alicho kuwa nacho mtoto ambacho mwanamke yoyo hawezi kujifunga kwa
njia ya kawaida
- kutokana na hari hiyo madakitari wa waliamua kumfanyia upasuaji na ndipo mtoto huyo wa kiume alipotolewa na alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa
Kwa
upande wake muuguzi mkuu wa hospital hiyo ya wilaya ya Mpanda Elexzanda
Kasagula alisema kuwa mwanamke huyo alifikishwa katika hospital hiyo
hapo juzi na kulazwa katika wodi ya wazazi baada ya kuonekana muda wake
wa kujifungua umefika
- hari ya Johari ambae amelazwa katika wodi ya wazazi inaendelea vizuri na wanasubiriwa ndugu zake ili wakabidhiwe mwili wamarehemu kichanga hicho kwa ajiri ya mazishi
- alisema hili ni tukio la pili ndani ya kipindi cha miezi mitatu kwa kuzaliwa watoto wa ajabu kwani miezi mitatu iliyo pita alizaliwa mtoto huku utumbo ukiwa nje juu t umbo
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment