HATIMAYE nguli wa sanaa za maigizo
Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ amelianika jimbo atakalogombea ubunge
mwaka 2015.
JB aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es
Salaam ambapo
alisema
macho yake yote yapo Mkoa wa Dar es Salaam ambao una majimbo nane.
JB: Niliposema natangaza kugombea ubunge
mwaka 2015 wengi waliamini ni maneno tu, lakini nia yangu ni sahihi.
Nitagombea na leo nasema jimbo langu lipo Mkoa wa Dar es Salaam.
Aliongeza
kuwa, jimbo atakalogombea litaendelea kubaki kuwa siri ya moyo wake na
meneja wake wa kampeni ambaye hakupenda kumtaja jina.
Majimbo
yanaounda mkoa wa Dar es Salaam katika uwakilishi bungeni ni Ukonga,
Ilala, Kinondoni, Segerea, Kawe, Kigamboni, Ubungo na Temeke.
Kiukweli
umefika wakati sasa wakurudisha fadila kwa mashabiki wangu nahitaji
kuwatumikia kwani na amini nikifanya hivyo hata kwa mungu nitapata
baraka alisema msanii huyo mwenye mashabiki wengi sana
Jb aliendelea
kuieleza thesupestarstz kuwa kugombea kwake ubunge kunaenda sambamba na
hali halisi anayoiona kwa wananch watanzania na kuongeza kuwa sasa
tunatakiwa kuwa na hofu ya mungu kwa wananch wetu wanaotuchagua kwa kura
nyingi wakiamini wamepata mkombozi matokeo yake wewe unawageuka ki
ukweli inauma sana.
Thesuperstarstz
imeongea na baadh ya wasanii wenzake kutaka kujua wanalichukuliaje
swala hilo ambapo wengi wameonyesha kumkubali jb na kusema kama
atafanikiwa kuwa mbunge basi utakuwa ni wakati mzuri sasa kwa wasanii
kupata mkombozi
|
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment