0



 Inafahamika kwamba umeme ndio chanzo cha maendeleo ya mji wowote kwani kukiwepo na umeme baadhi ya watu wata wekeza viwanda vidogo vidogo na pia mji utapiga hatua zaidi ya kumi mbele.Na kama hiyo haitoshi umeme ufanya eneo la mji fulani kuwa na mvuto sana tofauti na kutokuwepo kabisa.
     Wakazi wa Runzewe iliyopo wilaya wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita wanaiomba selikali kufikiria suala la umeme kwenye mji wao.Wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wamesema ghalama wanazotozwa na wanaogawa umeme binafsi gharama zao zimekuwa ziko juu sana, wamesema kuwa kwa wtumiaji wadogo kama matumizi ya kuchaji simu tu wenye vibanda wanalipa Sh 120000/-{Laki na ishilini }kwa mwezi mmoja na wengine ulipa Sh 150000/- hadi Sh 210000/- kwa mwezi mmoja tu. na wanaotumia majumbani ghalama zake uwa ni Sh 30000/- hadi Sh 50000/- kwa mwezi mmoja na hapo uwe na taa moja na tv tu na ukiwa na zaidi ya hapo ghalama inaongezeka mara dufu. Wameomba selikali wafanye mpango angalau waweke hata mashine kubwa zenye uwezo wa kutoa umeme kwa ghalama ndogo.Na wamemuomba Mbunge wao Pr Kaigi akishirikiana na Diwani wake  Yusufu wafanye jitihada kwa suala hilo.
   Pia wanamsifu sana Diwani wao kwa baadhi ya maendeleo aliyofanya mjini hapo.
 

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X