WABUNGE katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao
walihudhuria mafunzo ya kijeshi katika kambi tofauti za Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT), walipata msoto wa nguvu.
Kutoka
kushoto: Halima Mdee, Ester Bulaya na Neema Hamid.
Tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa kwamba wabunge hao wangepewa mafunzo
kwa kubembelezwa kutokana na nafasi zao, walikutana na msoto wa nguvu
mwanzo hadi mwisho.
Kuonesha jinsi ambavyo msoto ulikuwa wa nguvu,
katika kambi ya Tanga, siku tu ya utambulisho, mbunge wa Chadema (jina
tunalo), alizimia.
Vilevile, kwenye Kambi namba 832, Ruvu, Pwani,
Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine, alishindwa kuhimili kishindo cha
depo, hivyo akatoroka, japo mafunzo yenyewe yalikuwa ya muda wa wiki
tatu tu.
Baadhi
ya wabunge wakiwa katika pozi na wanajeshi wengine.
ILIKUWA KAZI KWELI
Siku ya kwanza tu ya kuripoti kambini, wabunge
wote walipigwa vipara na baada ya hapo, ilifuata awamu ya kupima afya.
“Jeshi ni jeshi tu, tulipimwa ukimwi bila hata kuandaliwa wala kupewa
ushauri,” alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria depo hiyo (jina tunalo)
kisha akaongeza: “Mfano mimi ningeambiwa kule kuna kupima ukimwi hata
nisingeenda, nilikuwa sijapima kama miaka saba, dah kule ni hatari.”
Mbunge
wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, akinyolewa nywele.
KUHUSU VIPARA
Mbunge mwingine alisema: “Walichotuweza ni ile
tunaripoti tu, tunanyolewa vipara halafu ndiyo taratibu nyingine
zinafuata. Kama wangekuwa wanatuonesha picha ya kile kitakachofanyika
kabla ya kutunyoa, wengi wetu tungetimka mapema.
“Tatizo unanyolewa
halafu ndiyo unapelekwa kupimwa ukimwi, sasa ukikataa kupima na una
kipara chako, mtaani utarudi vipi? Hata kunyoa, wengine tuliingia na
rasta, lakini wakatupiga upara wa wembe harakaharaka bila hata kungoja
kuzifumua.”
...Wakiwa
mazoezini.
MAFUNZO YANA FAIDA?
Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Umoja wa
Vijana wa CCM, Mkoa wa Mara, Ester Bulaya, alisema kuwa anashukuru
kupata mafunzo ya kijeshi, kwani yamemjenga kwa kiasi kikubwa.
“Japo
ni kazi lakini tunatamani muda uongezwe, maana wiki tatu zilikuwa fupi,
program ni nyingi, kwa hiyo tukatakiwa kufanya kwa pamoja,” alisema
Bulaya kisha akaongeza: “Imenijenga kweli, najiona mkakamavu mwenye
uwezo zaidi wa kutumikia wananchi.”
Kwa upande wa Mbunge wa Kawe
(Chadema), Halima Mdee, alisema: “Natamani kila mtu awe anapitia mafunzo
ya JKT, maana siyo tu yanakujenga kiukakamavu, bali pia yanakupa
uzalendo na ari ya kuwatumikia wananchi.”
...Wakiwa
katika picha ya pozi.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment