Wanawe rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson
Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu
kutoka katika makampuni anayoyamiliki.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo ya habari nchini
humo.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai
kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo
ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1
Mmoja wa wasaidizi hao, ambaye pia ni wakili wa
Mandela, George Bizos,amekana madai hayo.
Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa
kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa
ugonjwa wa mapafu pamoja na homa ya mapafu.
Mandela alilazwa hospitalini mara ya nne katika
kipindi cha miaka miwili.
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa
kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo
kwenye jina la Mandela hususan picha alizokuwa anachora akiwa jela.
Makaziwe na Zenani Mandela waliwasilisha kesi
mahakamani wakidai kuwa bwana Bizo, waziri wa nyumba, bwana Tokyo
Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally Chuene, hawakuwahi
kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya Harmonieux
Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings, kulingana na
gazeti la Star.
Pesa zinazotokana na makampuni hayo zinapaswa
kuwafaidi wanawe Mandela na yeye mwenyewe.
"Bizos, Chuene na Sexwale hawakuwahi kuteuliwa
rasmi kama washika dau katika kampuni hiyo.''
Bwana Bizos, wakili anayeheshimika sana na
ambaye pia ni rafiki wa karibu sana wa bwana Mandela, alisema kuwa
watajitetea vikali katika kesi hiyo.
Aliongeza kuwa wanawe Mandela walikuwa wanataka
kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa .
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment