
Mussa Yusuf
MSANII wa filamu, muziki na
vichekesho nchini, Mussa Yusuf 'Kitale', amechafuliwa katika ukurasa
wake wa Facebook juzi Jumanne. Akiongea na mtandao huu akiwa mjini
Kahama, Kitale amesema kuwa juzi Jumanne alipigiwa simu na mashabiki
wake wakilalamika kuhusu alichokiandika katika ukurasa wake wa facebook
ambapo kulikuwa na ujumbe uliokuwa ukiukashifu Ukristo. "Nimejisikia
vibaya sana baada ya kupigiwa simu na mashabiki wangu kuwa nameukashifu
Ukristo. Mimi ni Muislamu safi na siyo teja kama ninavyoigiza, siwezi
kukashifu dini yoyote, naomba radhi sana ndugu zangu kwa kilichotokea.
Kuna mtu aliingia katika akaunti yangu akaandika uchafu huo, na baadaye
alianza kuwatumia marafiki zangu ujumbe katika simu zao za mikononi
akiikashifu dini ya Kikristo kwa kujifanya yeye Kitale na yupo Dar
wakati mimi mwenyewe bado nipo Kahama," alisema Kitale.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment