Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema
ameachiwa kwa dhamana hivi punde
baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa
Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la
Arusha, Tanzania.
Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.

Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na
wanachama wa Chadema wanafanya
maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo
katika eneo la Ngarenaro.
Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za
kuzomea.
Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema
imefunguliwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.
Mwandishi wetu anasema kwamba kesi hiyo
imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu.
Endelea kuwa nasi kwa taarifa moto moto.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment