Kim amuita Barthez Stars...
KOCHA Mkuu Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha pili cha timu ya taifa, Taifa Stars, ambacho atakitumia kuangalia wachezaji anaoweza kuwaita kwenye kikosi cha kwanza huku jina la kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ likiwemo na mchezaji kutoka England.
Akizungumza kabla ya kutaja kikosi hicho jana, Kim alisema hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4, 2013.
Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, lakini hawajapata nafasi ya kucheza timu ya Taifa Stars.
“Leo (jana) ninatangaza timu ya pili ya Stars ambayo inaundwa na wachezaji wengi vijana wa umri chini ya miaka 20 na wachache ambao hawajapata nafasi ya kuichezea ile ya kikosi cha kwanza.
“Tofauti na vijana hao, pia nimeita wakongwe kama Barthez, Barnabas (Vicent) na David Mwantika kwa ajili ya kuwaangalia uwezo wao zaidi na kama nikiona wanafaa nitawapandisha kwenye timu ya kwanza,” alisema Kim.
Wachezaji walioitwa wataingia kambini Mei 2 hadi 6, mwaka huu. Walioitwa ni; Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta (Simba).
Viungo ni; Haruna Chanongo, William Lucian, Jonas Mkude, Edward Christopher, Abdallah Seseme, Ramadhan Singano (wote Simba), Mudathiri Yahya (Azam), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni; Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar) na Barthez.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment