
WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI
WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA
POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI
(80)
Watu
wawili wamenusurika
kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya
kahama mkoani
shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya
kishirikina.
Watu
hao waliojitambulisha kwa
majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi
wilayani
humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo
wakielekea
Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.
Katika
maelezo yao wazee hao
wamedai kuwa wameanguka baada ya kutokea
ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao
hawakuwafahamu
walikotoka na walikokuwa wanaelekea.
Sambamba
na hayo imeelezwa
kuwa wazee hao walikuwa uchi wakati wakianguka kabla ya kusaidiwa nguo
na mama
mmoja wa maeneo ya Kafe Latino barabara ya Mhongolo.
Jeshi
la Polisi la Wilayani humo likiri kutokeakwa
jambo jambo hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea na taarifa
zitatolewa
baadaye.
WAZEE WAKIWA HOI,HUKU WA KUSHOTO
AKIWA ANATEMA MATE OVYO KITUONI HAPO.
HAPA AKITEMA MAPOVU HUKU AKISEMA ANA
NJAA SANA.
BIBI AKIWA AKIWA HOI BAADA YA
KUDONDOKA USIKU WA LEO
HAPA BIBI AKISAIDIWA KUINUKA BABADA
YA KUVALISHWA NGUO NA WASALIMIA WEMA.
ASKARI POLISI WAKIWASAIDIA
KUWAPANDISHA KWENYE GARI.
HAPA WAKIPELEKWA KITUO CHA POLISI
MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA
MAJIRA PATRICK MABULA AKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA WALIOSHUHUDIA
TUKIO HILO.
HAPA NDIPO ENEO AMBALO WACHAWI HAO
WALIPODONDOKEA.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment