0

c 9b1f3
Bao dakika ya mwisho: David Luiz akifunga kwa mpira wa adhabu kuipa ushindi wa 2-1 Chelsea ugenini

BAO la dakika ya mwisho la mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja nyavuni la David Luiz limeipa ushindi wa mabao 2-1 Chelsea katika Nusu Fainali ya kwanza ya Europa League ugenini dhidi ya wenyeji Basle. 
Awali, alinusurika kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kudaiwa kucheza rafu.
 
 
Refa Pavel Kralovec alitoa uamuzi wa ajabu sana alipodai Luiz kamchezea rafu Cesar Azpilicueta kwenye eneo wakati hakucheza na akawapa penalti wenyeji wakapata bao la kusawazisha lililofungwa na Fabian Schar dakika ya 87.
 
 
Chelsea ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Victor Moses dakika ya 12.
Kikosi cha Basle kilikuwa: Sommer, Philipp Degen, Schar, Dragovic, Park, Fabian Frei, Salah/Degan dk78, El-Nenny/Zoua dk65, Die/Diaz dk61, Stocker na Streller. 
 
 
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Terry, Cole, Luiz, Hazard/Mata dk71, Ramires, Lampard/Oscar dk79, Moses na Torres. Katika Nusu Fainali nyingine, Fenerbace imeilaza 1-0 nyumbani Benfica, bao pekee la Korkmaz dakika ya 72.

ca 012b8
Luiz akishangilia bao.

cau a8cef
Victor Moses (kulia) akiifungia Chelsea

c1 52fa0
Fabian Schar akiifungia Basle kwa penalti bao la kusawazisha

c3 22659
Eden Hazard alikuwa nyota wa mchezo

c4 85eae
Rafa Benitez anataka kuipa Chelsea taji la Europa League msimu huu

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X