 |
Gari
lililokuwa limeubeba mwili wa msanii mkongwe wa muziki wa tarab,
marehemu Fatuma Binti Baraka 'Bi. Kidude', likiusafirisha kutoka katika
Kijiji cha Kihinani na kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho
ya mazishi yatayofanyika kesho mchana katika Kijiji cha Kitumba, Wilaya
ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
|
 |
Mwili
wa marehemu ukishushwa katika gari wakat ukiwasili nyumbani kwake,
Rahaleo kwa taratibu za mazishi yatakayofanyika kesho mchana na Kijiji
cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
|
 |
Ndugu,
Jamaa na marafiki, wakiubeba mwili wa marehemu Bi. Kidude wakati
ulipowasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa ajili ya matayarisho ya mazishi
yatakayofanyika kesho Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini
Unguja.
|
 |
Mrajisi
wa Baraza la Sanaa la Zanzibar, Khadija Batashi, akizungumza na
waandishi wa habari jinsi alivyoupokea msiba wa msanii mkongwe wa muziki
wa taraba nchini, Bi Kidude.
|
 |
Matayarishi ya mazishi ya msanii wa muziki wa tarab, Bi. Kidude yakiendelea nyumbani kwake Rahaleo, mjini Zanzibar.
|
 |
| Mjukuu
wa Bi. Kidude Omar Ameir, akiwasiliana na jamaa kwa ajili ya
kuwajulisha msiba wa marehemu Bi. Kidude, baada ya mwili wa marehemu
huyo, kuwasili nyumba kwake kwa ajilimatayarisho ya mazishi
yatakayofanyika kesho mchana baada ya Swala ya Adhuhuri, ambapo atazikwa
Kitumba. |
 |
Bi.
Maryam Hamdani akilakiwa na Bi. Sihaba wakati akiwasili nyumbani kwa
marehemu Bi. Kidude Rahaleo, mjini Zanzibar akiwa na majonzi.
|
 |
Waandishi
wa habari wakizungumza na Mfadhili Mkubwa wa Bi. Kidude, Maryam Hamdan,
kuhusiana na marehemu ambaye yeye alikuwa ni mtayarishaji na mratibu wa
safari za Bi. Kidude nje ya nchi na katika matamasha mbalimbali
aliyokuwa akihudhuria nje ya nchi wakati wa uhai wake.
|
 |
Meneja
wa Sauti ya BUSARA Zanzibar, Stella Steven, akizungumza na waandishi wa
habari, mjini Zanzibar kwenye msiba huo, kuhusiana na marehemu Bi.
Kidude ambaye alikuwa akidhaminiwa na Sauti za BUSARA katika matamasha
mbalimbali yaliokuwa yakiandaliwa na taasisi hiyo ya sanaa, jinsi
walivyopokea kifo chake kwa masikitiko makubwa na kuacha pengo katika
tasnia ya muziki wa taarab asilia Zanzibar.
|
|
(Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid wa ZanZinews)
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment