Jorge Mario Bergoglio(Pope Francis) akipewa salamu na Papa aliyejiuzuru Benedict 16 |
Kadinali
Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa
Papa. Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi
katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa.
Hii
ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza
mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi
yao. Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye
alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea
kuliongoza Kanisa Katoliki. Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku
ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne
kwa siku.
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne. Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment