0


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo alipofika kutoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta, aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam. Makweta enzi za uhai wake aliwahi kuwa Mbunge na Waziri katika wizara mbalimbali, hapa nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo alipofika kutoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta, aliyefariki dunia juzi jijini Dar es Salaam. Makweta enzi za uhai wake aliwahi kuwa Mbunge na Waziri katika wizara mbalimbali, hapa nchini.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Uratibu wa Bunge, William Lukuvi, akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa marehemu, huko Bunju, jijini Dar es Salaam. 
 Spika wa Bunge Mhe Anne Makinda akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali.
Mke wa Rais Mama Salma akiwafariji wana familia wa marehemu Jackson Makwetta ambaye kabla ya kufariki kwake juzi alipata kuwa Mbunge na waziri katika wizara mbalimbali.

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X