UCHAWI umetajwa kwenye mapenzi ya staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na ubavu wake wa sasa, Chuchu Hans.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mapenzi ya Ray kwa Chuchu ni makubwa
sana kiasi kwamba hayawezi kuwa ya hivihivi tu kwani msichana huyo ni
mtoto wa Kitanga anayejua jinsi ya kumshika mwanaume kama Ray.
“Unajua siku moja niliongea na mtu, sitaki kumtaja jina.
Akasema anaamini mambo ya ‘kiswahili’ yapo katika mapenzi ya wawili
hao, si rahisi Ray akawamwaga akina Johari (na Mainda) na kubaki na
Chuchu tu.
“Yule Chuchu ni mtoto wa
Kitanga, watoto wa Kitanga ni waja leo waondoka leo, wanajua mambo mengi
sana kuhusu mapenzi, wapo akina Mwakipesile walikwenda Tanga kufuata
biashara ya nazi hawakurudi Mbeya,” kilisema chanzo hicho.
“Kama mtakumbuka waandishi, siku moja kwenye magazeti yenu
mliandika kwamba Ray amesema hana mpango wa kumuoa Chuchu, lakini juzi
tu kamvisha pete ya uchumba kwa hiyo sasa uchumba wao ni rasmi.
“Halafu kama mtakumbuka tena katika habari ileile, mlimuuliza
Chuchu kuhusu madai ya Ray kwamba hana mpango wa kumuoa, alijibu Ray
hana ubavu huo, yaani wa kutomuoa. Sasa niambieni, mtu ambaye hana
mpango wa kumuoa demu, kwa nini amvishe pete ya uchumba?” kilihoji chanzo.
Kikaendelea: “Hata kwenye tasnia ya filamu, wengi wanasema
mapenzi ya Ray na Chuchu yana ‘kamzizi’ si bure maana jamaa ameoza
kuliko inavyotakiwa.”
Baada ya taarifa hizo, juzi Amani lilimsaka Ray na kubahatika
kukutana naye kwenye Gym moja iliyopo Kinondoni jijini Dar ambapo
alipoulizwa kuhusu madai hayo hakupenda kutoa ushirikiano wowote ule,
akasingizia anawahi hospitali ana Homa ya Dengu.
Chuchu alipatakana nje ya Meeda Club Jumamosi iliyopita ambapo alipoulizwa alisema:
“Kwanza nyie mbona mnapenda sana kuwafungukia watu bila wao kujifungukia wenyewe? Acheni watu wafunguke wenyewe bwana.”
Hata hivyo, ni kweli Chuchu Hans ana pete ya uchumba kwenye kidole kinachohusika.

Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment